Gathemane kwaya wakifanya huduma
Assacs kwaya wakitoa huduma
Ilikuwa ni siku nzuri sana Jumapili October,11-2015 katika kanisa la KKKT Manispaa ya Sumbawanga kushiriki katika huduma kwa njia ya uimbaji. Namshukuru Mungu kwa wema wake pia Mwinjilisti Aniset Msangawale na waumini wote kwa mapokezi mazuri waliyonipatia. Nimetambulisha Album yangu ya nyimba za Injili ''NILIPIGWA PICHA" na kuimba wimbo wa ALARM. Aidha kwaya mbalimbali ziliweza kutoa huduma zikiwemo zile za kanisa hilo na zingine mbili zilizokuwa zimealikwa kushiriki huduma ya uimbaji kwa siku hiyo.





